Shirika la Habari la Hawza – Ushauri wa Ayatollah Bahjat (ra) kuhusu kupokelewa dua ni huu:
"Mojawapo ya njia ya kisheria kwa ajili ya kupokelewa dua na kukidhiwa haja ni kwamba: Mtu mwenye haja au mwenye matatizo aombe dua na amuombe Mwenyezi Mungu ayaondoe matatizo yote yanayofanana na matatizo yake kutoka kwa Waumini wa kiume na wa kike wote walio na matatizo hayo; au atimizwe haja yoyote inayofanana na haja yake kwa waumini wote; kwani katika hali hiyo, malaika humuombea dua yeye binafsi, na dua ya malaika huwa inakubaliwa."
Maoni yako